Marekani inataka Korea Kaskazini kumuachilia Bae

Image caption Kenneth Bae

Mjumbe mmoja wa Marekani anatarajiwa kuwasili Korea Kazkazini hii leo katika ziara inayolenga kuirai serikali ya taifa hilo kumwachilia Kenneth Bae, aliyekamatwa nchini humo mwezi Novemba, mwaka uliopita.

Katika ziara ya kwanza iliofanywa na afisa wa ngazi ya juu kutoka Marekani katika kipindi cha miaka miwili, balozi Robert King anatarajiwa kuomba kuwachiliwa kwa Bae kwa misingi ya kibinaadamu.

Raia huyo wa Marekani ambaye ni kiongozi wa dini alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela na kazi ngumu kwa kile Korea Kazkazini inadai ni uvamizi.

Bwana Bae alilazwa hospitalini mapema mwezi huu baada ya uzani wake kupungua kwa ghafla.