Kerry asema sarin ilitumiwa Damascus

John Kerry, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Marekani, John Kerry, anasema Marekani ina ushahidi wake unaoonesha kuwa sarin ilitumiwa katika silaha za kemikali zilizotumiwa kushambulia kitongoje cha Damascus.

Akizungumza kwenye televisheni, alisema nywele na damu iliyopata Marekani kutoka watu wa mwanzo waliokuwako kwenye shambulio la mwezi uliopita, inaonesha ilikuwa na sarin.

Na Syria imemuelezea Rais Obama kuwa anasita-sita na amechanganyikiwa kwa sababu ameakhirisha hatua ya kuingilia kati kijeshi, hadi baraza la Congress limeidhinisha hatua hiyo.

Naibu waziri wa mashauri ya nchi za nje wa Syria, Faisal Makdad, amesema shambulio lolote la Marekani dhidi ya Syria litakuwa shambulio dhidi ya Iran.