Mabomu yaripua hoteli mbili Mogadishu

Mogadishu, Somalia

Polisi nchini Somalia wanasema mashambulio mawili ya mabomu mjini Mogadishu yameuwa watu kama 15.

Polisi walieleza kuwa mabomu hayo yaliripuka kwenye mkahawa uitwao The Village ambao unapendwa na waandishi wa habari na maafisa wa vikosi vya usalama, pamoja na hoteli Muna, ambako wabunge wengi hukaa.

Hoteli zote mbili ziko karibu na ikulu ya rais.

Hakuna aliyedai kuhusika na mashambulio hayo, lakini hoteli zote mbili zimewahi kushambuliwa na wapiganaji wa Kiislamu, al Shabab.