Watoto wa Somalia wahimizwa kwenda shule

Watoto wa Somalia

Wakuu wa Somalia wameanzisha kampeni ya kuwapeleka shule watoto milioni moja.

Kampeni hiyo iitwayo "nenda shule" imeanza mjini Mogadishu na katika miji ya Somaliland na Puntland, yaani Hargeisa na Garowe, kwa msaada wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa, Unicef.

Baada ya vita vya miongo mwili, Unicef inasema asili-mia-40 tu ya watoto wanakwenda shule Somalia - kati ya viwango vya chini kabisa duniani.

Unicef inasema mradi huo utawapa robo ya watoto wasiokwenda shule fursa ya kusoma.

Mradi utagharimu dola 117 milioni.