Meli yenye Bhangi ilisajiliwa Zanzibar

Image caption Mmea wa Bhangi

Polisi nchini Tanzania wamethibitisha kuwa meli iliyokamatwa Jumamosi katika bahari ya Mediterranea ikiwa na mizigo ya Bhangi yenye thamani ya dola milioni sabini na nane, ilikuwa imesajiliwa Zanzibar.

Wafanyakazi tisa waliokuwa kwenye meli hiyo wanaosemekana kuwa raia wa Misri na Syria, waliwasha moto meli hiyo na kuruka baharini, ingawa baadaye waliokolewa.

Maafisa wa ushuru wa Italia walioinasa meli hiyo iliyokuwa kwenye ufuo wa Sicily baada ya kupata taarifa, walisema kuwa mizigo iliyokuwa na mizigo ya Bhangi yenye tani thelathini, ilipakiwa kwenye meli hiyo bandarini Uturuki ingawa haijulikani ilikokuwa inapelekwa.