Swala la siasa kali Somalia kujadiliwa

Image caption Kundi la wapiganaji la Al Shabaab

Kikao maalum cha Wasomi wa kisomali na walimu wa dini kinaendelea katika mji ,mkuu wa Somalia Mogadishu Kujaribu kutanzua tatizo la waisilamu wenye msimamo mkali wa kidini .

Cha mno ni uelewa wa ufasiri unaotumika na makundi ya kiislamu yenye msimamo mkali wa kidini kama vile lile la Al-Shabab.

Na kwa siku chache zijazo zaidi ya wajumbe 160 watakuwa wakitafsri na kutathmini tafsiri mwafaka kwa nia ya kuhamasisha jamii kuhusiana na tofauti ya tafsiri ya kidini na tofauti nyinginezo.

Hayo yanajiri baada ya kundi la Al shaabab kukiri kuhusika katika shambulizi la bomu lililosababisha vifo vya watu 15 mjini Mogadishu.