Ruto na Sang wakana mashtaka ICC

Image caption Naibu rais wa Kenya William Ruto

Kesi dhidi ya naibu rais wa Kenya William Ruto, imeanza kusikilizwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC huko Hague.

Bwana Ruto anayetuhumiwa kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007, alikana mashtaka yote dhidi yake. Vile vile mshtakiwa mwenza mtangazaji wa redio Joshua Arap Sang pia alikana mashtaka.

Rais Uhuru Kenyatta ambaye pia anatuhumiwa kuhusika na ghasia hizo anatarajiwa kufika mbele ya mahakama hiyo mwezi Novemba.

......Ikiwa unafuatilia kesi hiyo unaweza kutupa maoni yako kuhusu inavyoendesjwa kwenye ukurasa wetu wa facebook bbcswahili kisha tutayaweka maoni yako hapa.......

13:10 PM: Wakili wa

12:24 PM: Wakili Stenberg ambaye anaendelea kuelezea mahakama kuhusu ushahidi wao amesema kuwa Ruto alisambaza silaha kwa vijana ambao wangefanya mashambulizi dhidi ya watu wa kabila hasimu waliokuwa wanaishi katika mkoa wa Rift Valley

Image caption Ruto akiwa na Joshua Arap Sang wakati kesi dhidi yao ilipowasilishwa katika mahakama ya ICC

12:13 PM Wakili Steynberg wa upande wa mashtaka amesema kuwa Ruto aliahidi kuwazawadi wale ambao wangefanya uhalifu katika mikutano ambayo vijana walihudhuria kwa wengi wakati wakipangia vurugu baada ya uchaguzi

12:01PM Upande wa mashtaka unasimulia ambavyo unapanga kuthibitisha kuwa kesi yao ni ya uhakika, ushahidi utakaotolewa , na nani atakayetoa ushahidi huo. Mashahidi inasemekana watawataja wahusika wengine kwenye kesi hiyo hasa walioshirkiana na washtakiwa kufanikisha mipango yao.

11:55AM: Upande wa mashtaka kupitia kwa wakili Steynberg umeiambia mahakama kuwa kila mshukiwa anakabiliwa na mashtaka matatu ya kuwalazimisha watu kuondoka makwao kwa lazima, mauaji na kuchochea ghasia

11:51AM: Bensouda aambia mahakama kuwa amekuwa na wakati mgumu sana kukusanya ushahidi wa kesi yake akisema kuwa wengi wa mashahidi wamejiondoa katika kesi hiyo wakisema wanahofia maisha yao na kuongeza kuwa baadhi pia wamehongwa ili wasitoe ushahidi wao

11:41 AM: Fatou Bensuda mwendesha mkuu wa mashtaka katika mahakama hiyo aelezea mahakama kuhusu tuhuma zinazowakabili Ruto na Sang kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007-2008. Bansuda amesema kuwa Ruto alifanya mauaji kwa sababu za kisiasa huku Sang akimsaidia kuchochea ghasia ili kumsaidia kufanikisha ajenda yake ya kuingia mamlakani

11:35AM Joshua Sang pia amekanusha mashtaka yote dhidi yake

Image caption Ghasia za baada ya uchaguzi Kenya mwaka 2007

11:33 AM Ruto amekana mashtaka yote aliyosomewa na upande wa mashtaka kuwa alihusika na uhalifu dhidi ya binadamu , mauaji, dhulma na kuwaondosha watu makwao kwa lazima

11:24: AM Naye Joshua alisomewa mashtaka dhidi yake ya kuchochea ghasia katika mkoa wa Rift Valley kwa kutumia kituo cha redio alichokuwa anafanyia kazi kueneza chuki na ukabila

11:23 AM Ruto asomewa mashtaka dhidi yake na kuambiwa kuwa alihusika na mauaji ya watu katika mkoa wa Rift Valley

11:20AM :Kesi dhidi ya mshukiwa mkuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya Naibu Rais William Ruto imeanza kusikilizwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC .

11:00AM: Wahusika wote kwenye kesi hii kutoka upande wa naibu rais Ruto, mshukiwa mwengine Joshua Arap Sang na upande wa mashtaka wake Fatou Bensauda walijitambulisha mahakamani kwa ombi la mmoja wa majaji kwenye jopo la majaji