Upinzani Syria wakana makubaliano

Mpiganaji wa Syria katika mji wa Deir Ezzor, mashariki mwa nchi

Mkuu wa kijeshi wa upinzani nchini Syria, Jenerali Selim Idris, amekataa makubaliano baina ya Marekani na Urusi kuhusu silaha za kemikali za Syria.

Akizungumza na waandishi wa habari nchini Uturuki, Jenerali Idris alisema makubaliano hayo hayatamaliza msuko-suko wa sasa.

Amesema upinzani utaendelra na vita.

Aliwashauri Wamarekani wasidanganywe na pendekezo la Urusi ambalo alisema linakusudia kuvuta wakati.

Inaarifiwa kuwa mapambano yanaendelea baina ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa upinzani katika vitongoje vya Damascus vinavyodhibitiwa na wapiganaji.

Walioshuhudia wanasema ndege za jeshi la Syria zinafanya mashambulio.