Wakimbizi kutoka Syria waingia Utaliana

Wakimbizi wa Syria

Walinzi wa pwani wa kusini mwa Utaliana wamewaokoa wakimbizi kama 500 kutoka mashua mbili katika masaa 24.

Wengi wa wakimbizi hao ni kutoka Syria.

Wakimbizi 170, wengi wao wanawake na watoto, wamepelekwa bara la Utaliana.

Na wengine kama 300 waliokolewa Ijumaa usiku karibu na mwambao wa Sicily na kupelekwa mji wa Syracuse.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na wakimbizi linasema idadi ya Wasyria wanaokimbilia Utaliana imeongezeka sana na Wasyria zaidi ya 3,000 wameingia katika siku 40 zilizopita.