Brazzaville yatuma askari zaidi CAR

Wapiganaji wa Seleka  mjini Bangui waliponyakua madaraka mwezi March

Congo-Brazzaville imezidisha zaidi ya mara dufu idadi ya askari wake katika kikosi cha kuweka amani katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Congo-Brazzaville imechukua hatua hiyo baada ya ghasia kuzidi ambazo zimeuwa watu zaidi ya 60 juma lilopita.

Wanajeshi 200 zaidi wametumwa huko na hivo kufanya jumla ya wanajeshi wake kufikia 350.

Jamhuri ya Afrika ya Kati imetibuka tangu wapiganaji wa kundi la Seleka kumpindua Rais Francois Bozize mwezi March.

Serikali mpya inayoongozwa na mpiganaji wa zamani, Michel Djotodia, imekuwa ikipigana na wanajeshi watiifu kwa Bwana Bozize.