Askofu aachiliwa huru Nigeria

Askofu Ignatius Kattey

Kiongozi mmoja wa kanisa la Anglikana la Nigeria ambaye alitekwa nyara zaidi ya majuma mawili yaliyopita, ameachiliwa huru.

Afisa wa polisi alisema Askofu Ignatius Kattey aliachiliwa huru jana usiku na yuko katika hali tulivu.

Askofu alitekwa karibu na nyumbani kwake katika mji wa Port Harcourt eneo la Niger Delta pamoja na mkewe, lakini yeye aliachiliwa huru mapema.

Utekaji nyara unatokea mara nyingi katika Niger Delta kudai kikombozi lakini haijulikani kama kililipwa katika kisa hiki.