Msukosuko wa kifedha ulileta maafa

Image caption Nchi nyingi za Ulaya ndizo zilikumbwa na msukosuko mkubwa wa fedha

Watafiti wamesema kuwa msukosuko wa kifedha ulioshuhudiwa duniani mwaka 2008 ulisababisha kuongezeka kwa visa vya watu kujitoa uhai duniani,hususan wanaume.

Kwenye utafiti huo ambao matokeo yake yalichapishwa katika jarida la afya la Uingereza,watafiti kutoka Uingereza na Hong Kong walisema kuwa takriban wanaume elfu tano zaidi walijitoa uhai mwaka wa 2009 kuliko idadi ya kawaida.

Waliongezea kuwa vijana wa Ulaya na wanaume wenye umri wa makamu wa Marekani walikumbwa na uhaba mkubwa wa ajira wakati huo.

Hata hivyo watafiti hao wameonya kuwa athari za msukosuko huo wa kifedha kwa maisha ya watu yalikuwa mabaya sana hasa kwa sababu watu wengi sana walijaribu kujitoa uhai.