Huwezi kusikiliza tena

Ahadi ya mamilioni kwa Somalia

Imekumbwa na miaka zaidi ya ishirini ya vita na serikali kuporomoka, lakini sasa mkataba mpya umefikiwa kwa watu wa Somalia.

Muungano wa Ulaya umeahidi kuipa Somalia zaidi ya dola milioni 860 kama msaada kwenye kongamano lililofanyika mjini Brussels.

Wengi wanatumai kuwa pesa hizi zitaweza kuondoa Somalia katika hali mbaya na kuipa sura mpya katika kipindi cha miaka mitatu pekee. Lakini changamoto nyingi zinasalia.