Risasi zafyatuliwa kati ya Nairobi

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya  akiapishwa mjini Nairobi mwezi Aprili

Ripoti kutoka Nairobi, Kenya, zasema kwamba watu waliokuwa na silaha wamefyatua risasi katika eneo la biashara katikati ya mji mkuu huo.

Inaarifiwa kuwa polisi waliobeba silaha wako katika eneo hilo.

Shirika la habari la Reuters linaarifu kuwa mpiga picha mmoja aliona watu wamelala chini tuli, hawatikisiki.

Hadi sasa hakuna taarifa rasmi kama kuna watu waliokufa.