Wajerumani wachagua bunge jipya

Wafuasi wa Angela Merkel wa chama cha CDU wakati wa kampeni

Wananchi wa Ujerumani wanapiga kura kuchagua bunge jipya.

Uchaguzi huo utaamua iwapo Bibi Angela Merkel atarudi tena madarakani kwa muhula wa tatu.

Chama chake cha Christian Democrats (CDU) kinatarajiwa kushinda idadi kubwa ya viti kushinda vyama vengine.

Hata hivyo itategemea iwapo washirika wake wa chama cha Free Democrat katika serikali ya mseto, watapata kura za kutosha kuingia bungeni.

Ama sivyo, Bibi Merkel huenda akalazimika kuunda serikali na chama kikuu cha upinzani cha Social Democrats ambacho alishirikiana nacho katika muhula wake wa kwanza.