Matukio katika jengo la Westgate

Image caption Vikosi vya usalama vinavyopambana na magaidi walio ndani ya jengo hilo

Katika ukurasa huu tutakupasha moja kwa moja matukio yanavyojiri katika jengo la Westgate ambako inaarifiwa vikosi vya usalama vimezingira jengo hilo na hata kudhibiti sehemu ya jengo zima. Ikiwa uko karibu na uwanja huo unaweza kutupasha hali unavyiona kupitia kwa ukurasa wetu wa facebook bbcswahili

14:03 Mkuu wa polisi David Kimaiyo asema kuwa vikosi vya usalama vinakaribia kudhibiti hali na vimeingia ndani kabisa ya jengo hilo kiasi cha kuwaokoa baadhi ya mateka

14:00 PM: Milipuko zaidi yasikika katika jengo hilo

13:54: Mwandishi wa BBC Idriss Situma aliye katika eneo la Westgate anasema duru zinaarifu kuwa vikosi vya usalama vya Kenya vinasema kuwa ndivyo vimelipua sehemu ya jengo kujaribu kuingia ndani kabisa ya jengo hilo

13:52 PM Magari ya Ambulance yaobnekana yakienda katika eneo la shambulizi pamoja na magari ya zima moto. Vikosi vya usalama vinawataka watu kuondoka karibu na eneo la operesheni hiyo ili kuwawezesha kufanya kazi yao

13:49 pm: Moshi mkubwa mweusi waonekana ukitoka juu ka juu katika jengo hilo haijulikani nini kilichosababisha

13:19 pm Moshi mkubwa unaonekana ukitoka katika jengo la Westgate ambako wapiganaji wa Al Shabaab wanawazuilia mateka wakenya ambao idadi yao haijulikani

13:12 PM Viongozi wa kidini watoa taarifa kulaana kitendo cha Al Shabaab

12:30 PM: Milipuko zaidi na milio ya risasi imesikika katika jengo la Westgate huku vikosi vya usalama vikifanya jitahada za misho kuwa