Ndovu 81 wauawa kwa sumu Zimbabwe

Image caption Zimbabwe ni moja ya nchi Afrika zinazosifika kwa mbuga zake

Maafisa wa wanyama pori nchini Zimbabwe wamesema kuwa takriban ndovu 81 wameuawa kutokana na sumu ilio mwagwa katika eneo la malisho ya ndovu hao.

Tangazo hilo linajiri baada ya maafisa kuzuru mbuga ya wanyama pori ya Hwange mwishoni mwa juma lililopita.

Sumu hiyo ambayo hutumiwa katika migodi ya dhahabu ilimwagwa katika eneo hilo na wawindaji haramu.

Tayari wawindaji haramu 9 wamekamatwa.

Zaidi ya ndovu 40 walipataikana wameuawa katika mbuga hiyo mwezi uliopita.