Mwanawe generali afungwa jela China

Image caption Li Tianyi ni mwanawe Generali mkuu katika jeshi la China

Mahakama nchini China imemhukumu mwanawe mmoja wa majenerali wakuu wa jeshi miaka kumi gerezani kwa kosa la ubakaji

Majaji katika kesi hiyo walisema kuwa mahakama Li Tianyi, 17, na wenzake wanne walimbaka mwanamke katika hoteli moja mjini Beijing mwezi Februari baada ya kupokea vinywaji.

Alikuwa amekana kuwa na uhusiano wowote wa kingono na mwanamke huyo ambaye alidai alikuwa ni hanithi.

Li Tianyin ni mwanawe generali wa jeshi, Gen Li Shuangjiang, anayesifika kwa uimbaji wake wa nyimbo za kizalendo kwenye televisheni.

Mamake Li Tianyi, Meng Ge pia anasifika kwa uimbaji wake katika jeshi la taifa.

Kesi hiyo ilisikika katika mahakama ya Haidian Kaskazini Magharibi mwa Beijing. Watetezi wengine pia walihukumiwa kifungo cha kati ya miaka mitatu na 13.

Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Li Tianyi, ambaye anajulikana kama Li Guanfeng, kuhusika katika tukio ambalo limeghadhabisha umma.

Mnamo mwaka 2011, alizuiliwa kwa mwaka mmoja baada ya tukio moja la barabarani.

Alikuwa anaendesha gari ambalo halikuwa na nambari ya usajili pale alipowashambulia kwa maneno mwanamume na mkewe waliokuwa ndani ya gari na hata kuwazuia.

Aliwatusi wawili hao na kuwakemea mbele ya umma ulioshangazwa na tabia yake akiwaonya dhidi ya kuita polisi.

Babake aliomba radhi kwa kosa hilo

Kesi dhidi ya Li Tianyi ilisababisha hasira miongoni mwa watu wanaowaona watoto wa watu mashuhuri kama wasio na maadili awenye kuhujumu sheria.