China kuchimba visima vya mafuta Uganda

Image caption uchimbaji mafuta ukifanywa na kampuni ya (CNOOC)

Kampuni ya kitaifa inayomilikiwa na China ya Offshore Oil, (CNOOC) imeshinda kandarasi yenye thamani ya dola bilioni 2 kujenga kiwanda cha mafuta nchini Uganda.

Kiwanda hicho kinaaminika kuwa na uwezo wa kuzalisha mitungi milioni 635 za mafuta.

Hatua hii ni ya uwekezaji ya hivi karubini kuchukuliwa na makampuni ya China katika sekta kigeni ya mafuta na gesi.

Makampuni ya China, yamekuwa yakitaka kuekeza katika sekta ya kawi ili kukidhi mahitaji yake ya kiuchumi.

Kampuni hiyo itajenga kiwanda hicho kwa kipindi cha miaka minne.

Aidha kiwanda hicho kina uwezo wa kuzalisha kati ya mitungi 30,000 hadi 40,000 ya mafuta kila siku.

Ukuwaji wa haraka wa uchumi wa China katika miaka ya hivi karibuni, imesababisha kuongezeka kwa mahitaji ya mafuta , na kuifanya kuwa nchi inayotumia mafuta kwa wingi duniani.

Mahitaji hayo yanatarajiwa kuongezeka hata zaidi huku uchumi wake ukiendelea kukuwa.

Lakini China inategemea sana bidhaa za kutoka nje kuweza kukidhi mahitaji yake.

Kutokana na hilo, makampuni ya China yanatafuta sana kuekeza katika sekta ya gesi na mafuta.

Mwaka jana kampuni hiyo ilikubali kulipa dola bilioni 15.1 katika kununua kampuni ya mafuta ya Nexen nchini Canada.