Obama azungumza na Rouhani

Rais Rouhani na Obama

Kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 30, viongozi wa Marekani na Iran wamezungumza moja kwa moja.

Rais Barack Obama na mwenzake wa Iran, Hassan Rouhani, wamezungumza kwa simu kwa muda wa robo saa; na kwa mujibu wa Bwana Obama walieleza azma yao ya kutatua mzozo wa muda mrefu kuhusu mradi wa nuklia wa Iran.

Ujumbe kwenye mtandao wa Twitter kutoka ofisi ya Bwana Rouhani ulionesha hisia kama hizo.

Taarifa kutoka Iran zinaonesha kuwa tukio hilo limefurahiwa nchini humo, hasa kati ya washauri wakuu wa Bwana Rouhani.