13 wafariki katika ajali ya ndege Nigeria

Ndege iliyokuwa imewabeba watu 27 imeanguka baada ya kukumbwa na hitilafu ya injini, muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege mjini Lagos.

Duru zinasema kuwa watu 13 wamefariki huku watu kadhaa wakipata majeraha mabay.

Ndege hiyo ya shirika la ndege la Associated Airlines, iliyokuwa na uwezo wa kubeba watu 30 ilianguka muda mfupi tu baada ya kuruka na kulipuka.

Aidha ilikua inaelekea mjini Akure Kusini Magharibi mwa nchi, kwa mujibu wa msemaji wa shirika la udhibiti wa safari za angani nchini humo.

Injini ya ndege ilikumbwa na hitilafu na kuisababisha ndege kuanguka na kuteketea.

Hata hivyo hakuna taarifa za kuthibitisha idadi ya watu waliofariki.

Ndega hiyo iliruka mwendo wa saa mbili unusu kutoka katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Murtala Mohammed

Maafisa walisema kuwa ndege hiyo ilianguka karibu na bomba la mafuta katika uwanja huo.

Haijulikani ikiwa mafuta hayo ndiyo yalisababisha ndege kulipuka.

Shahidi mmoja alimbia BBC kuwa alisikia mlipuko mkubwa uliofatiwa na moshi mkubwa ukifuka kutoka katika sehemu ya ajali hiyo.

Maafisa wa usalama waliharakisha kwenda katika eneo la ajali na kuanza kuwaokoa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo.