Khamenei hakufurahi na ziara ya Rouhani

Rouhani akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Kiongozi wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, amesema kuwa anaunga mkono juhudi za kidiplomasia za Iran za hivi karibuni, lakini baadhi ya yale yaliyotokea katika ziara ya rais mpya, Hassan Rouhani, kwenye Umoja wa Mataifa juma lilopita hayakuwa sawa.

Kwenye tovuti yake Ayatollah Khamenei ananukuliwa akisema kwamba Iran bado haina matumaini kuhusu Marekani.

Aliielezea serikali ya Marekani kwamba haiaminiki, inajiona, na haina busara.

Mwandishi wa BBC anasema inaonesha maneno hayo yanakusudiwa kuzimua matumaini yaliyotokeza juma lilopita baada ya Rais Rouhani kuzungumza na Rais Obama kwa simu.