Wanajeshi watano wauawa Misri

Image caption Kuna wasiwasi kuwa wanajeshi na vikosi vya usalama vinalengwa kwa mashambulizi la Misri

Watu waliojihami nchini Misri wamewaua wanajeshi watano katika eneo la Mkondo wa Suez mjini Ismailiya.

Maafisa wa usalama wanasema kuwa washambuliaji waliwafyatulia risasi wanajeshi hao walipokuwa wanaketi karibu na kizuizi cha barabarani kaskazini mwa mji huo.

Maafisa wa usalama wanasema kuwa wanajeshi wamekuwa wakilengwa kwa mashambulizi katika siku za hivi karibuni.

Wakati huohuo, mlipuko mkubwa uliotokana na bomu liliokuwa limetegwa ndani ya gari limelipuka na kuwaua watu wawili.