Utaliana itazidisha doria Mediterranean

Wanajeshi wakisaidia katika uokozi, Lampedusa

Utaliana itazidisha doria za wanajeshi kusini mwa bahari ya Mediterranean, baada ya mamia ya wakimbizi kuzama wakati mashua zilizowabeba kwenda mrama hivi karibuni.

Waziri Mkuu wa Utaliana, Enrico Letta, alisema operesheni ya pamoja baina ya jeshi la wanamaji na lile la wanahewa itaanza hapo kesho.

Alisema hatua hiyo inahitajika kwa sababu katika siku za karibuni bahari imechafuka.

Ukosefu wa utulivu Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati, unawafanya watu wengi kujaribu safari hiyo ya hatari, kuvuka Mediterranean kuelekea Ulaya - mara nyingi katika mashua zilizojaa mno na ambazo siyo imara.

Wengi wanatokea Libya wakielekea kisiwa cha Lampedusa, Utaliana.