Hajj yaelekea ukingoni Mecca

Image caption Hajj ni mojawapo ya nguzo za dini ya kiisilamu.

Mamia ya waumini wa kiisilamu walikusanyika katika bonde la Minna nchini Saudi Arabia kushirki katika kitendo cha kurushia mawe minara inayoashiria shetani katika moja wapo na hatua za mwisho za Hajj.

Kama waisilamu, kote duniani walisherehekea siku kuu ya Eid al-Adha, ambapo wanachinja mnyama au kutoa kafara kwa Mungu wakiwa wamevalia vazi maalum la Hajj walirushia mawe minara inayoashiria shetakani.

Ingawa idadi ya mahujaji ilipungua kutoka watu milioni 3.2 waliohudhuria Hajj mwaka jana, bado watu wengi walifanya Hajj kama mojawapo ya nguzo muhimu za dini ya kiisilamu.

Takriban mahujaji milioni,1.5 waliofanya hajj mwaka huu mahujaji milioni 1.38 walitoka katika nchi 188 za kigeni. Na walianza shughuli ya kutupa vijiwe kwenye minara inayoashiria shetani kuanzia asubuhi mapema lakini idadi ya watu iliendelea kuongezeka.

Shughuli hiyo itaendelea hadi siku ya Ijumaa, lakini mahujaji wanaofanya kwa kasi wanaweza kuimaliza kwa siku moja.

Aidha kitendo hicho kinatokana na alivyofanya Mtume Ibrahim aliyemrushia vijiwe shetani aliyekuwa anamshawishi kutomchinja mwanawe Ishmael kama alivyoamrishwa na Mungu.

Hii leo waliendelea na kitendo hicho walichokianza siku ya Jumatatu huku viongozi wa nchi kadhaa wakibeba mabango na bendera za nchi yao.

Zamani watu wengi walikuwa wanajeruhiwa sana wakati wa kitendo cha Minna lakini watawala wa Saudi Arabia wameweza kudhibiti hali kwa kuruhusu idadi ndogo ya watu wanaokuja Mecca