Gavana wa Cicily atangaza hali ya hatari

Image caption Maiti za wahamiaji kutoka Afrika katika kisiwa cha Lampedusa

Gavana wa Kisiwa cha Cicily nchini Italia, ametangaza hali ya hatari kwa sababu ya idadi kubwa ya wahamiaji kinachokabiliana nao.

Amri hiyo itaruhusu utoaji fedha kwa ajili ya wafanyakazi wa misaada ambao watasaidia kuwahudumia mamia ya wahamiaji kutoka Afrika na Syria.

Maafisa wa Italia wamesema wahamiaji 370 wameokolewa kutoka katika mashua matatu katika bahari kati ya Libya na Sicilia Jumanne.

Wahamiaji wote walikuwa wakipelekwa katika kisiwa cha Lampedusa.

Uokoaji wa sasa umekuja siku moja baada ya Italia kutangaza kuongeza doria kufuatia vifo vya mamia ya wahamiaji ambao wanasafiri katika mashua zenye msongamano mkubwa wa abiria.

Watu wapatao 33 wamekufa Ijumaa wakati mashua yao ilipozama kati ya Malta na kisiwa cha Lampedusa.