Mripuko wauwa watu kadha nje ya Damascus

Wanajeshi wa serikali mjini Damascus

Wanaharakati nchini Syria wanasema watu kama 16 wamekufa kwenye mripuko mkubwa katika kituo cha ukaguzi cha jeshi katika viunga vya mji mkuu Damascus, eneo lenye wakaazi wengi Wakristo na Wadruze.

Mripuko huo ulitokea katika lango la kuingia eneo la Jaramana ambalo ni ngome ya rais Bashar al Assad, karibu na mji wa Al-Melha unaodhibitiwa na wapiganaji.

Mripuko huo ulizusha mapambano zaidi.