Moto wazidi kuwa mkali Australia

Athari za moto New South Wales, Australia

Serikali ya Australia imetangaza hali ya dharura katika jimbo la New South Wales, ambako wazima moto wanaopambana na moto wa vichakani wanajizatiti kwa hali inayozidi kuwa mbaya.

Hali ya dharura inawapa wakuu idhini ya kulazimisha watu wahame majumbani mwao na kuzima umeme ikihitajika.

Watabiri wa hali ya hewa wanasema joto litazidi na upepo kuzidi kasi na hivo kuupepea huo moto katika siku zijazo.

Mkuu wa kitengo cha wazima moto mashambani katika jimbo la New South Wales, Shane Fitzsimmons, aliwaambia waandishi wa habari kwamba anataraji hali kuzidi kuwa ya hatari.