Facebook yaondoa picha zinazoogofya

Image caption Facebook yazuia picha zenye kuogofya

Siku chache tu baada ya mtandao wa Facebook kusema kuwa utawaruhusu watu kuweka filamu za video zinazoonyesha ghasia,imeondoa filamu moja ya video ya mwanamke anayekatwa shingo.

Tangazo hilo la hapo jana kwamba itaondoa marufuku hiyo kwa mda,miongoni mwa video za ghasia ilizua malalamishi mengi kutoka kwa uma.

Facebook sasa imesema itapanua vigezo vyake ili kubaini iwapo filamu za video zitawekwa katika mtandao huo au la.

Mwandishi wa BBC anayesimamia maswala ya Technologia amesema hatua hiyo inawakilisha mabadiliko muhimu yalioshinikizwa na uma.