Jeshi DRC linadai kuelekea ngome ya M23

Mwanajeshi wa serikali na ushanga wa risasi, karibu na KIbumba

Ripoti kutoka Jamhuri ya Demokrasi ya Congo zinaeleza kuwa mapigano bado yanaendelea kwa siku ya tatu huku jeshi la serikali likidai kuwa limeuteka mji wa Kibumba, mashariki mwa nchi, na kuwatoa wapiganaji wa kundi la M23.

Kibumba, ilioko kilomita 20 kaskazini ya Goma, ndiko walikokimbilia wapiganaji baada ya kikosi cha Umoja wa Mataifa, MONUSCO, kuwatoa katika mji wa Goma.

Msemaji wa jeshi anaarifiwa kueleza kuwa wameteka miji mengine piya na kwamba jeshi limejigawa na linaelekea kusini upande wa Rutshuru.

Mapigano yalizuka Ijumaa siku chache baada ya mazungumzo ya amani ya mjini Kampala, Uganda, kuvunjika..