G4S yatuhumiwa kwa ukatili Afrika Kusini

Image caption Kamuni ya ulinzi ya G4S imakanusha madai ya ukatili dhidi ya wafungwa

Wafanyakazi wa jela moja la Afrika Kusini la wahalifu sugu na ambalo linalindwa na kampuni ya ulinzi ya Uingereza G4S , wametuhumiwa kwa kufanya ukatili wa kiwango cha kushtua.

Serikali ya nchi hiyo sasa imeamua kudhibiti ulinzi wa jela hiyo ya Mangaung ya kuanzisha uchunguzi.

Hatua hii inajiri baada ya wafungwa kulalamiika kuwa kupigwa kwa nguvu za umeme na kulazimishwa kudungwa sindano hata hivyo G4S inakanusha madai hayo ikisema kuwa hakuna ushahidi kuwa wafanyikazi wake wanatekeleza vitendo hivyo.

BBC imepata video kutoka katika gereza hilo lenye ulinzi mkali ambapo milio ya nguvu za umeme inasikika .Inaonyesha pia mfungwa mmoja akikataa kupewa matibabu

Watafiti wa Wits Justice Project kutoka chuo kikuu cha Wits mjini Johannesburg wanasema kuwa wamekusanya ripoti za wafungwa karibu 30 kuhusiana na kupigwa kwa nguvu za umeme na kuchapwa katika utafiti wao wa mwaka mmoja

Mwandishi wa BBC Andrew Harding anasema kuwa serikali ya Afrika Kusini inasema kuwa hali katika gereza hilo lenye ulinzi mkali ya Mangaung ni ya kushtua sana

“Wengine walisema kuwa walizirai waliposhindwa kustahimili uchungu wa nguvu za umeme,” alisema Ruth Hopkins ,mwanahabari wa mradi wa Wits Justice

Alisema kuwa wafungwa walilalamika kuhusu kuvunjika kwa mikono na miguu na majeraha mengine makuu.

Mmoja wa aliyekuwa mfungwa kwa gereza hilo aliambia BBC kuwa nguvu za umeme zilitumika kuwatesa ,vilevile askari aliyefutwa kazi aliongezea kuwa wafungwa walimwagiliwa maji ili kuongeza uzito wa nguvu za umeme.

“Madai yoyote ya yakiripotiwa kwetu ,ambayo ni ya kesi ya kipekee inatubidi kuyashughulikia vilivyo”

Kulingana na mwandishi wa BBC wa Afrika Andrew Harding ,wakili wa baadhi ya wafungwa hao alishutumu tabia ya wafanyikazi katika gereza hilo kufanya ukatili bila kujali.

G4S hata hivyo imedai kuwa kuwepo na purukushani katika gereza hilo ni kwa sababu ya mzozo wa ajira. Zaidi ya askari 300 walifutwa kazi mwezi huu baada ya kushiriki mgomo

Nontsikelelo Jolingana,ambaye ni kamishna wa vitengo vya marekebisho aliambia BBC kuwa kitengo chake kimeanza uchunguzi rasmi kuhisiana na madai hayo .

Shirika la magereza ya Afrika Kusini mwezi jana lilitangaza kuwa wanachukua wanadhibiti ulinzi katika gereza hilo lililo katika mkoa wa Central Free State kwa muda baada ya shirika la kibinafsi la usalama kushindwa kulisimamia vyema gereza hilo.

Andy Baker, ambaye ni mkuu wa G4S Afrika alisema kuwa kuwadunga wafungwa sindano si jukumu la G4S bali ni la wafanyikazi wa afya.

Alipoulizwa kuhusu madai ya kutumia nguvu za umeme na kupigwa didhi ya wafungwa alisema kuwa “hakujawahi kutokea jambo hilo”.