Markel:Obama hakujulishwa kuhusu Udukuzi

Image caption Obama amesema kuwa hakuwa na habari kuhusu udukuzi dhidi ya simu ya Markel

Mkuu wa shirika la ujasusi nchini Marekani NSA hakuzungumzia madai ya udukuzi wa simu ya Chansela wa Ujerumani Angela Markel na rais Barack Obama .

Kwa mujibu wa msemaji wa shirika hilo, Gen Keith Alexander hakuwahi kumtajia Obama kitendo cha kudukua simu ya Markel, kinachodaiwa kufanywa na shirika hilo.

Vyombo vya habari nchini Ujerumani vinasema kuwa Marekani imekuwa ikinasa mawasiliano ya kwenye simu ya Markel tangu mwaka 2002, na kuwa Rais Obama alifahamishwa kuhusu habari hiyo mwaka 2010.

Kashfa hii imesababisha mgogoro mkubwa wa kidiplomasia kati ya nchi hizo kuwahi kushuhudiwa katika historia ya mataifa hayo.

Ripoti kwenye gazeti moja la udaku nchini Ujerumani zinasema kuwa Genrali Alexander mwenyewe aliwahi kumhabarisha Obama kuhusu kitendo cha kudukua simu ya Markel.

Hata hivyo jarida hilo limesea kuwa kulingana na taarifa kutoka ndani ya NSA Obama hakuwahi kusitisha kitendo hicho, kwani alitaka kujua kila kitu kuhusu Marke kwani hakumuani sana.

Hata hivyo taarifa hizo zimekanushwa vikali na shirika hilo zikisema kuwa Obama hakuwahi kujulishwa kuhusu kitendho hicho na kuwa taarifa zinazosema vinginevyo ni za kupotosha.

Obama hata hivyo ameripotiwa kumwambia Bi Markel kuwa hakujua chochote kuhusu udukuzi huo wakati walipokutana.

Ujerumani inatuma maafisa wake wakuu wa ujasusi nchini Marekani wiki ijayo ili kushinikiza kufanywa uchunguzi katika madai ya udukuzi wa simu ya Bi Markel ambayo yamesababisha ghadhabu nchini humo.