Makamanda 2 wa Al Shabaab wauawa Barawe

Image caption Wakaazi wa Barawe wanasema walionda ndege ikipaa angani baada ya kurusha kombora kubwa

Shambulizi la angani Kusini mwa Somalia dhidi ya kundi la Al Shabaab limewaua viongozi wawili wa kundi hilo. Hii ni kwa mujibu wa wenyeji wa mji wa Barawe.

Shambulizi hilo liliharibu gari la wanamgambo hao waliokuwa wanasafiri kati ya miji ya Jilib na Barawe, inayoonekana kuwa ngome ya kundi hilo.

Mapema mwezi huu Marekani ilifanya mashambulizi yaliyotibuka wakitaka kumkamata kamanda wa kundi hilo.

Al-Shabaab ni kundi rasmi linalohusishwa na kundi la kigaidi la al-Qaeda- Afrika Mashariki.

Duru za kijeshi nchini Kenya ziliambia BBC kuwa jeshi lao lilivamia mji wa Jilib, na huenda baadhi ya wanamgambo walijeruhiwa.

Hata hivyo, wadadisi wanasema kuwa huenda sio wanajeshi wa Kenya waliofanya mashambulizi ya angani.

Wakaazi wa mji wa Jilib, ulio umbali wa kilomita 120 Kaskazini mwa mji wa bandarini wa Kismayo, waliambia BBC kuwa huenda makomando hao wawili waliuawa kwa kutumia ndege zisizo na rubani.

Mmoja wa waliouawa alikuwa mtaalamu wa silaha wa kudni hilo anayejulikana kama Anta,mmoja wa kundi hilo alibia sjirika la habari la AP.

Hii leo nilisikia mlipuko mkbwa na kuiona ndege isiyo na rubani ikiishia angani, angalau makomanda wawili waliuawa,’’ alisema mkaazi mmoja wa eneo hilo kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters.

"Niliona gari likiteketea na wanaume wengi wa Al Shabaab walikuja katika eneo hilo. Na pia niliwaona wakibeba maiti za wawili hao.’’

''Ndege hiyo ilirusha kombora kubwa na magari mengi yalikuwa mbele yangu ingawa ni gari la magaidi hao lililoshambuliwa tu.''

Angalau watu 67 waliuawa mwezi jana wakati kundi la Al shabaab liliposhambulia jengo la Westgate mjini Nairobi.

Makomando wa Marekani walivamia mji wa Barawe baada ya shambulizi la Nairobi, ingawa walilazimika kuondoka baada ya masambulizi yao kutibuka.

Makomando hao walitaka kumkamata kamanda mmoja mkuu wa kundi hilo Abdukadir Mohamed Abdukadir, anayejulikana kwa jina lengine kaka Ikrima.