Wakimbizi kutoka DRC wakimbilia Uganda

Image caption Wakimbizi wa DRC wengi wana kimbilia usalama wao nchini Uganda

Melfu ya wakimbizi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, wameingia nchini Uganda, huku majeshi ya serikali ya DRC yakipambana vikali na waasi wa M23.

Makabiliano makali kati ya pande hizo mbili yamepamba moto huku kukiripotiwa kutokea mashambulizi ya maombora karibu na mji wa Bunagana ulio kati ya mpaka wa DRC na Uganda.

Msemaji wa shirika la kuwahudumia wakimbizi la UNHCR, alisema kuwa wakimbizi elfu mbili wamevuka na kuingia Uganda hii leo na kuifikisha idadi ya wakimbizi hao hadi elfu tano.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa mapema wiki hii alisema kuwa kundi la waasi la M23 lsio tisho tena la kijeshi kufuatia ushindi kadhaa wa jeshi dhidi ya waasi hao ambapo waliweza kuthibiti miji iliyokuwa imetekwa na waasi hao.

Aliongeza kuwa waasi hao wametoeroka maeneo ya Bunagana na kwamba sasa wako katika kipnade kidogo cha ardhi karibu na mpaka wa Rwanda.

Wanajeshi wa DRC wakisaidiwa na jeshi la Umoja wa Mataifa( MONUSCO) walifanikiwa kudhibiti kambi ya kijeshi ya Rumangabo siku ya Jumatatu