Israel yafanya mashambulizi ya angani Syria

Image caption Vifaru vya Israel tayari kwa mashambulizi dhidi ya Syria ikiwa itafanya visivyo

Ndege za kivita za Israel zimefanya mashambulizi katika mji wa pwani wa Syria wa Latakia.

Hii ni kwa mujibu wa afisaa mkuu wa Marekani alisema kuwa shambulizi hilo lililenga makombora ya Urusi yaliyokuwa yananuiwa kupelekwa kudni la wapiganaji la Hezbollah.

Latakia ni ngome ya kisiasa ya Rais Bashar al-Assad, na pia kuwa mji muhimu ambako jamii yake ya Alawite inatoka.

Israel, inasemekana kufanya angalau mashambulizi matatu ya angani dhidi ya Syria mwaka huu pekee.

Taarifa hii inajiri huku kikundi cha wataalamu wa silaha za kemikali kutoka shirika la OPCW waliokuwa na jukumu la kuharibu vifaa vya silaha za kemikali vya Syria, kusema kuwa limekamilisha kazi yake siku moja kabla ya makataa iliyotolewa.

Hatua ya shirika hilo ilitokana na makubaliano yaliyofikiwa kufuatia madai yaliyokanushwa na serikali ya Syria kuwa majeshi yake yalitumia nguvu pamoja na silaha za kemikali katika maeneo ya raia , na pia baada ya Marekani na Ufaransa kutishia kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya Serikali ya Syria.

Afisaa huyo alisema kuwa mashambulizi yalifanyika Jumatano na kuendelea hadi Alhamisi.

Hata hivyo Syria na .Urisi zingali kutoa tamko lolote kuhusu madai hayo.

Israel imekuwa ikisema kuwa itachukua hatua ikihisi kuwa silaha za Syria, ziwe za kemikali au za kawaida zinapelekewa wapiganaji katika eneo hilo hasa kundi la wapiganaji la Hezbollah