Siasa zilivyoibua mgawanyiko Misri

Baada ya aliyekuwa Rais wa Misri Mohammed Morsi kuondolewa mamlakani na jeshi la nchi hiyo Tarehe 3 Julai, kufuatia msururu wa maandamano, wafuasi wake walikusanyika Cairo eneo la Nasr city.

Maandamano hayo yaliyoendelea kwa muda wa wiki sita nje ya msikiti al-Rabaa-Adawiya yalisitishwa na jeshi na kuleta maafa kwa mamia ya watu.

Sasa wakaazi wengi kutoka eneo hili hupatikana katika sehemu ya kuuzia na kununua magari kila wiki. Soko hiyo huwa na maelfu ya watu kutoka sehemu tofauti za Misri ambao hununua ama kuuza magari.

Mengi yakitarajiwa baada ya kesi ya Morsi kuanza, masuala ya kujadiliwa sasa si maendeleo na bei ya bidhaa tu bali nini hasa hatma ya siku za usoni.

Siku za hivi karibuni makundi ya kiislamu yamendeleza maandamano katika mji mkuu wa Cairo, Alexandria na miji mingine ya Misri.

Hata baada ya viongozi wengi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood ambalo Rais huyo wa zamani ni mwanachama wake kutiwa nguvuni, inasemekana kupanga maandamano mengine kupinga kutiwa nguvuni kwa kiongozi wao.

Soko la magari la kila wiki huvutia mjini Cairo huvutia watu wengi kutoka maeneo mbalimbali ya Misri.

Msanii mmoja kutoka mji wa Cairo amekuja kuangalia magari ili kujiliwaza kidogo.

Mohammed Nur ambaye ni muislaamu anakerwa kwamba Rais aliyechaguliwa na watu kwa njia ya kidemokrasia aliondolewa mamlakani na anapanga kushiriki maandamano ya kumtetea Morsi.

Image caption Wafuasi wa Mosri waliandamana kumuunga mkono wakati kesi yake ikianza kusikilizwa Misri

"kwanza kabisa, hii ilikua mapinduzi, Jukumu letu ni kurekebisha kwa njia yoyote.Niliwapoteza marafiki zangu wawili kwa rabsha hizi na polisi, haturudi nyuma kamwe baada ya kumwaga damu hivi." asema Nur

"Tutafanya kila juhudi kuzuia kesi hii kuanza kwa sababu Rais Morsi hatapata haki katika kesi hii.Nina uhakika Mosri hakufanya kosa lolote."

Kupata haki?

Wanunuzi wengine wana maoni tofauti na hayo na wanaunga mkono kuhukumiwa kwa kiongozi huyo wa kundi la Kiislamu kwani anashukiwa kuwachochea wafuasi wake kuwaua wandamanaji mwaka jana.

" Idara yetu ya mahakama ni yenye haki na usawa, Morsi amefanya uhalifu mwingi na watu wengi walikufa wakati wa uongozi wake. Anafaa kuhukumiwa kifo" anasema Heba Fathallah mfanyi kazi wa umma ambaye hupo sokoni na familia yake.

Wamisri wengi walisherekea sana Julai tarehe 3 wakati Mosri aliondolewa mamlakani.

"Nilikua katika barabara za Alexandria tarehe 3 Juni na watoto wangu pamoja na wajukuu, nilikua na furaha sana kwamba Morsi alikua ameondolewa baada ya mwaka moja tu"

Anakubaliana pia na masharti makali iliyowekewa na jeshi ambalo linaunga mkono Serikali ya muda inayoongozwa na Waziri mkuu Hazem el-Beblawi, ambayo imezuia maandamano yoyote ya kundi la Muslim Brotherhood nakuwapokonya mali zao.

"Serikali ya Beblawi ina kila haki ya kuanza upelelezi dhidi ya Kundi la Muslim Brotherhood. Wameikosea nchi" asema Fathallah

"Wanataka kumrejesha Morsi na hiyo haiwezekani kamwe"

Maandamano yanaendelea

Image caption Hali ya usalama ilidhibitiwa na vikosi vya usalama kote Cairo

Inatarajiwa kwamba katika siku za usoni uhusiano baina ya Wamisri utaendelea kupotea na kuleta uhasama zaidi.

Mama mmoja mwenye umri wa makamo kutoka Giza, Abda al-Basir hapendi kuzungumzia siasa siku hizi. "Unaunga mkono Morsi .

Kama tu Wamisri wengine, alimpigia kura Morsi katika kinyang"anyiro cha urais lakini akapoteza imani naye kwani alishindwa kukabiliana na tatizo la uchumi, uhusiano wa watu na mpango wako wa kuifanya Misri nchi ya Kiislamu.

"sasa namuunga mkono Sisi kwa yale amefanya mpaka sasa" Bi. Abd al-Basdhir anaongezea " Nafkiri watu wengi kutoka mirengo yote miwili wameshauwawa, najua kundi la Muslim Brotherhood wamefanya makosa mengi lakini huwezi kuwaondoa namna hii. Yafaa kuwa na suluhisho, wanafaa kujumuishwa katika ratiba"

Mtu mmoja mwenye umri wa takriban 30 anasema kuwa " Familia yangu inahofu kama kundi la Brotherhood litatimuliwa na kwenda mafichoini na kupanga mashambuliuzi ya mabomu katika maduka na misikitini"

"kwafaa kuwa na mazungumzo nao, tunafaa kuwaacha waendelee na shughuli zao za kujitolea,kuwasaidia maskini na kutoa mafunzo misikitini lakini si kushughulika na siasa.