Israel, 'mshukiwa mkuu wa mauaji ya Araffat'

Image caption Mjane wa Arafat anasema ana uhakika kuwa mumewe aliuawa na Israel

Maafisa katika utawala wa Palestina, wanasema kuwa mshukiwa pekee wa mauaji ya aliyekuwa kiongozi wa Palestina Yasser Arafat ni 'Isreal.'

Madai haya yanakuja baada ya wanasayansi kusema kuna ushahidi wa kuonyesha kuwa maiti ya Araffat ilionyesha kuwa na dalili za kiwango kikubwa cha mionzi ya Polonium.

Mkuu wa kamati iliyobuniwa na Wapalestina kuchunguza kifo cha Arafat kilichotokea mwaka 2004, alisema kifo cha Araffat kilitokana na mauaji ya kupangwa

Alisema kuwa uchunguzi utaendelea kufanywa ili kuthibitisha maelezo yote kuhusiana na sakata hiyo.

Israel imekuwa ikikanusha madai ya kuhusika na mauaji ya Arafat.

Mjane wa hayati Arafat, amesema kuwa anaamini ripoti iliyotolewa hivi karibuni kuhusu kifo cha Araffat , ni dhihirisho kuwa aliuawa.

Hata hivyo, alisema kuwa mumewe alikuwa na maadui wengi, kote duniani na hangeweza kumtuhumu mtu yeyote.

Araffat alifariki hosipitalini mjini Paris mwaka 2004, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Wataalamu katika hospitali ya Lausanne, nchini Switzerland, walifanyia utafiti mifupa ya Arafat baada ya kuifukua Novemba mwaka 2012 na kusema kuwa ulikuwa na kiwango kikubwa sana cha sumu aina ya Pollonium.

Baadhi ya matokeo ya uchunguzi huo bado hayajachapishwa.