Tendulkar aagwa kwa tuzo kubwa

Sachin Tendulkar akiaga washabiki wake

Mwanakrikiti wa India, Sachin Tendulkar, ametunikiwa tuzo ya daraja ya juu kabisa kwa raia wa nchi yake, Bharat Ratna.

Tangazo hilo lilitolewa saa chache baada ya Tendulkar kumaliza kucheza mechi yake ya mwisho katika mechi za kimataifa.

Katika mechi hiyo India iliishinda uzuri timu ya West Indies kwenye mechi ya pili ya Test cricket mjini Mumbai.

Amepata sifa ya kuwa mmoja kati ya wachezaji wa kirikiti hodari kabisa kuwahi kuonekana kwenye mchezo huo, na ndiye mwana-michezo wa kwanza kupata tuzo hiyo ya Bharat Ratna.

Tendulkar ambaye ametimia miaka 40, anaacha krikiti baada ya kupata centuries nyingi kabisa kwenye krikiti ya kimataifa.