Bacteria sugu ni tishio kubwa

Dawa za antibiotics zinazouzwa Afghanistan

Tume ya wataalamu wa afya imeonya kuwa aina sugu ya vidudu vya bacteria ni moja kati ya tishio kubwa kabisa katika matibabu.

Katika taarifa iliyoandikwa kwenye jarida la kisayansi, The Lancet, wataalamu wanatoa wito mataifa yashirikiane ili kupambana na tishio hilo.

Itahitajika hatua kuchukuliwa pamoja na kupunguza idadi ya dawa za antibiotics ambazo madaktari wanawaandikia wagonjwa, na kuyapa motisha makampuni ya madawa kutengeneza dawa mpya.

Wataalamu hao wanaonya kuwa bila ya antibiotics, matibabu mengi, kutoka upasuaji hadi kutumia kemikali kutibu saratani - hayo hayatowezekana.

Na vifo kutokana na magonjwa ya kuambukiza katika nchi zilizoendelea vinaweza kurudi katika viwango kama vile vya awali ya karne ya 20.

Piya wataalamu wanasema gharama za matibabu huenda zikapanda sana.