Kimbunga chasababisha maafa Marekani

Image caption Kimbunga nchini Marekani chasababisha uharibifu mkubwa

Kimbunga kikali kimeyakumba maeneo kadha ya Marekani, kikiharibu majengo na magari katika majimbo ya Illinois, Indiana na Kentucky.

Watu wapatao watano wameuawa katika kimbunga hicho na inahofiwa kuwa mamia ya watu huenda wamejeruhiwa katika kimbunga hicho kikali.

Idadi kubwa ya watu wanasemekana kunasa katika majengo.

Wataalam wa hali ya hewa wanasema kimbunga hicho kitaathiri watu milioni 53 katika maeneo hayo.