China yaongeza ukanda wa anga ya ulinzi.

Image caption Kisiwa cha Senkaku au Diaoyu

Japani imefanya kile ambacho imekiita upingaji mkubwa dhidi ya China kufuatia maamuzi ya serikali ya Beijing kuanzisha ukanda wa anga ya utambuzi wa ulinzi katika eneo lenye mzozo wa maji katika bahari ya mashariki ya Uchina.

Waziri wa ulinzi wa Uchina amesema ndege zitakazokuwa zikiingia katika eneo hilo zitatakiwa kutoa taarifa za awali kabla ya kupita katika eneo hilo na kudumisha mawasiliano kwa kujibu maswali yatakayohitajika kutoka kwa waongozaji wa ndege.

Eneo hilo la ukanda wa ulinzi linahusisha visiwa vya Senkaku au Diaoyu ambavyo vimekuwa vikiongoza katika kukuwa kwa mzozo baina ya mataifa hayo mawili.