ICC yawakamata washirika wa Bemba

Image caption Bambe alikuwa naibu rais wa DRC na alikamatwa kwa tuhuma za za uhalifu wa kivita

Washirika wanne wa aliyekuwa naibu rais wa DRC, Jean-Pierre Bemba, wamekamatwa kwa madai ya kuhitilafiana na ushahidi dhidi ya Bemba katika kesi inayomkabili katika mahakama ya ICC.

Mahakama hiyo imethibitisha kuwa washukiwa wanne waliokamatwa ni pamoja na mawakili wa Bemba, pamoja na aliyekuwa karani wake.

Kesi dhidi ya kiongzoi huyo wa zamani wa waasi, imekuwa ikiendelea tangu Novemba mwaka 2010, ambapo anatuhumiwa kwa makosa ya mauaji , ubakaji na uporaji katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo

Mahakama ya ICC katika taarifa yake imesema kuwa washukiwa hao pia waliwasilisha stakabadhi bandia kwa mahakama hiyo.

Jean Pierre Bemba ni kiongozi wa upinzani pamoja na kuwa kiongozi wa waasi ambaye alifikishwa Hague kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

ICC imetoa vibali vya kukamatwa kwa watu 5 akiwemo Bemba, lakini pia, mawakili wake wawili, shahidi mmoja na mbunge kutoka kwa chama chake walikamatwa.

Wanatuhumiwa kuwa sehemu ya mtandao wa watu waliowasilisha stakabadhi bandia kwa mahakama ya ICC pamoja na kuwapa mlungula baadhi ya mashahidi ili watoe ushahidi wa uongo katika kesi dhidi ya Bemba.

Jean Pierre Bemba amezuiliwa Hague tangu mwaka 2008 kwa makosa anayodaiwa kuyafanya katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati,kati ya mwaka 2002-2003. Washirika wake walikamatwa na polisi nchini DRC, Ufarnsa , Ubelgiji na Uholanzi.

Mahakama inasema kuwa watapelekwa Hague jkatika muda mfuypi ujao.

Afisaa mmoja wa ICC aliambia BBC kuwa ikiwa watapatikana na hatia huenda watkatumia kifungo cha miaka mitano gerezani