Watuhumiwa Westgate wanyimwa dhamana

Image caption Watuhumiwa wanne wa shambulio la Westgate, Kenya

Mahakama nchini Kenya imewawanyima dhamana watuhumiwa wanne, wanaoshitakiwa kuhusika na shambulio katika kituo cha maduka cha Westgate mjini Nairobi, Kenya.

Mahakama hiyo imetoa uamuzi wa kutowapa dhamana kwa sababu ya usalama na uwezekano wa kuingilia ushahidi wa kesi hiyo.

Watuhumiwa hao wanne wanaosemekana kuwa ni wageni, wanashtakiwa kwa kuwasaidia watu waliofanya shambulio, ambapo watu 67 waliuawa na wengine 200 kujeruhiwa.

Watuhumiwa hao wamekana mashitaka dhidi yao.

Kikundi cha al-Shabab kinachohusishwa na kikundi cha ugaidi cha al-Qaeda- kilidai kuhusika na shambulio hilo.

Watu walioshitakiwa wametajwa kuwa ni Mohammed Ahmed Abdi, Liban Abdullah, Adnan Ibrahim na Hussein Hassan.

Tarehe 22 Septemba,2013 kikundi cha wapiganaji wa Somalia cha al-Shabab kinasema kinahusika na shambulio hilo.