Mamilionea wa Ethiopia,watoa wapi utajiri?

Image caption Kilimo ndio moja ya chanzo cha utajiri wa mamilionea Ethiopia

Afrikani ni bara linalosemekana kua mbioni kujikuza kiuchumi. Pamoja na hilo inasemekana sio uchumi tu unaonawiri bali pia idadi ya matajiri inaongezeka. Sio matajiri tu bali mamilionea

Kwa sasa kunao wa Ethiopia elfu mbili mia saba wanaoaminiwa kuwa na mali ya zaidi ya dola milioni moja.

Hii ni mara mbili ya idadi ya mamilionea waliokuwepo nchini humo miaka mitano iliyopita.

Inaaminiwa kuwa wengi wao wamejipatia fedha nyingi kutoka kwa kilimo utengenezaji bidhaa na biashara inayonoga katika sekta ya usafiri.

Angola, Zambia, Ghana na Nigeria pia zimetajwa kua na ongezeko kubwa la mamilionea.

Hata hivyo, kuongezeka kwa idadi ya mamilionea sio kumaanisha kuwa pesa zimesambazwa katika nchi.

Mwandishi wa ripoti hiyo Andrew Amoils, ametoa mfano wa Nigeria na Angola, kuwa mamilionea hao wanatawala kiasi kikubwa cha rasil mali za nchi kwa hivyo kuongezeka kwa idadi yao haiwafaidi raia kwa jumla.

Athari kubwa imekuwa kuelekeza juhudi zote sasa kwa kukuza na kuwapa uwezo zaidi wale raia wa kipato cha kadri, badala ya kujaribu kuweka usawa katika umiliki wa mali katika nchi.

Baadhi ya wadadisi wa uchumi wanaamini kuwa jambo la muhimu zaidi katika kulenga kukuza uchumi wa nchi kwa muda mrefu ni kuwezesha jamii ya kipato cha kadri watakaoweza kununua bidhaa za matumizi ya starehe mbali na bidhaa zile muhimu za uhai.

Hata hivyo kwa mujibu wa ripoti hiyo, licha ya kile kitakachotokea kwa raia hawa wa kipato cha kadri, bado idadi ya mamilionea inaendelea kukua.