Kauli yako kuhusu kifo cha Mandela

Image caption Nelson Mandela

Viongozi duniani wameendelea kutuma rambirambi zao kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.

Kifo cha Mandela kilitangazwa hapo jana Alhamisi saa za usiku naye Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliyesema kuwa Afrika Kusini inaomboleza kumpoteza kiongozi huyo waliyemuenzi sana kama mtoto wao , baba yao na kiongozi wa taifa hilo.

Mandela alifariki nyumbani kwake mjini Johanesburg na alikuwa ameugua homa ya mapau kwa muda mrefu.

Na wewe pia unaweza kutuma ujumbe wako kupitia ukurasa wetu wa Facebook ambao kisha nitauweka kwenye mtandao wa bbcswahili

Ingia kwenye ukurasa wetu wa facebook uweze ujumbe wako kufuatia kifo cha Nelson Mandela.

11:00 am:Charles Charlloh Yabuna wa Kakamega, Kenya anasema kupitia Facebook kua Wafrika kwa jumla tunaomboleza kifo cha mzalendo wetu

10:57 am : Ahamba Bokyo yupo Durban na kupitia Facebook anasema maombolezi yanaendelea salama kila mtu yuko kimia na machungu moyoni

10:40 AM: Adili Mwasomola kwenye ukurasa wake waFacebookamesema >natokea Kurasini DSMd TZ "katika afrika MANDELA ni mmoja wa viongozi walioifanya AFRIKA isiwe nyeusi TENA bali iwe sehemu salama kwa kuishi kila mtu bila kuwepo ubaguzi..... APUMZIKE KWA AMNI YOOOTE.... MBELE YAKE NYUMA YAKE

10:35 am: Ulimboka Lugano kupitia ukurasa wake wa Facebook anasema ameanza kumsikia Mandela akiwa anamalizia uongozi wake, na alitarajia kua Mandela angekaa madarakani kama rais kwa muda mrefu lakini kumbe nia yake haikuwa kuongoza bali kumkomboa mwana Afrika kusini kutoka katika ubaguzi wa rangi, namkumbuka kwa kitendo hicho cha kipekee, pia namkumbuka kupitia kusoma kwa roho yake isiyo kata tamaa pamoja na ugumu na kukosekana kwa uhuru wa mtu mweusi kutoka kwa serikali ya makaburu aliweze kuimarisha jeshi lake la 'Umkontho we sizwe'.

10:25 am: Albert Ottaru kupitia ukurasa wa facebook amesema Mandela ni shujaa wa mapambano ya utu wetu. Daima ataishi mioyoni mwetu. Apumzike kwa amani.

10:25 am Dakika chache zilizopia Malkia wa Uingereza Elizabeth ameelezea kushtushwa sana na kifo cha Mandela na kusisitiza kuwa mangaza wa Mandela utaendelea kunga'a nchini Afrika Kusini.