Serikali yajitenga na kesi ya ubakaji Somalia

Image caption Mwanamke huyo amedaiwa kusema uongo kuwa alibakwa

Serikali ya Somalia imesema haiwezi kuhusishwa na kesi ya mwananamke ambaye amehukumiwa kifungo jela baada ya kusema kwamba alibakwa, ikisema hili ni suala la kisheria.

Msemaji waserikali Ridwaan Haji amesema polisi na mahakama walifanya uchunguzi wa kina, ambao matokeo yake ni kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka kumi na tisa kuhukumiwa kifungo jela na waandishi wawili wa habari walioripoti habari hiyo nao pia wakahukumiwa.

Mwananamke huyo ambaye amehukumiwa miezi sita kifungo cha nyumbani, atabakia nyumbani kwake kipindi chote hicho. Amesema alibakwa akiwa ameelekezewa bunduki na wanaume wawili.

Sio mara ya kwanza kwa mwanamke Somalia kudai kuwa amebakwa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii