Nyumba ya Askofu Tutu yavamiwa

Image caption Desmond Tutu aliwakaripia wananchi wa Afrika Kusini alipokuwa anahutubia kwenye ibada ya Mandela

Wezi wamevunja na kuingia nyumbani kwa Askofu mstaafu Desmond Tutu.

Polisi wamesema wizi huo ulifanyika wakati bwana Tutu akiwa katika ibada ya Nelson Mandela Mjini Johannesberg.

Inaarifiwa Tutu aliibiwa vitu vyake wakati akiwa anahudhuria ibada maalum ya kumuaga Hayati Nelson Mandela siku ya Jumanne.

Aidha wameelezea kuwa uvamizi ulifanyika nyumbani kwake mjini Cape Town Ahamisi jioni baada ya kutoa hotuba katika ibada ya Mandela siku hiyo.

Ibada hiyo ilifanyika katika uwanja wa FNB mtaani Soweto.

Wizi na uvamizi wa nyumba za watu ni jambo la kawaida nchini Afrika Kusini ambako visa vya uhalifu viko juu sana.