Kenya yasherehekea miaka 50 ya Uhuru

Kenya inasherehekea miaka 50 ya uhuru walioupata chini ya utawala wa Uingereza.

Mamia ya raia na wageni mbali mbali wamehudhuria katika sherehe hizo zilizofanyika katika mji mkuu wa Nairobi.

Wageni mbali mbali pamoja marais wa mataifa mbali mbali wamehudhuria sherehe hizo akiwemo rais Nigeria Godluck Jonathan wa Nigeria, Jakaya Kikwete wa Tanzania, Joseph Kabila wa DRC, Pierre Nkurunziza wa Burundi, Ali Bongo wa Gabon, Mahinda Rajapaksa wa Sri Lanka.

Usiku wa kuamkia Alhamis bendera ya Kenya ilipandishwa katika eneo hilo hilo siku bendera ya uhuru ilipopandishwa wakati nchi hiyo inapata uhuru katika bustani ya Uhuru Desemba 12, 1963.

Siku hiyo ya uhuru Rais Jomo Kenyatta, baba yake rais wa sasa Uhuru Kenyatta alitawazwa kuwa kiongozi wa nchi hiyo.