Mandela amiminiwa heshima za mwisho

Image caption Polisi walikuwa na wakati mgumu kutokana na msongamano mkubwa wa watu waliofika kutoa heshima zao kwa Mandela

Mamia ya watu hii leo wamepata fursa ya mwisho kutoa heshima zao za mwisho kwa Hayati Nelson Mandela ambaye ,mwili wake uko katika jengo la kitaifa la Union mjini Pretoria.

Walikuwa miongoni mwa watu wa mwisho mwisho 50,000 kuuona mwili wa Mandela katika jengo la Union ambako mwili wa Mandele umelazwa.

Maafisa wanasema kuwa 100,000 walifika kumuaga Mandela kwa siku tatu zilizopita.

Jeneza la Mandela hata hivyo liliondolewa kutoka sehemu hiyo baada ya milango kufungwa nyakati za jioni.

Mwili wa Mandela utasalia kuwa mjini Pretoria usiku kucha na hatimaye kutakuwa na hafla maalum ya viongozi wa ANC nao kutoa heshima zao za mwisho kwa Mandela katika mojawapo ya kambi za jeshi siku ya Jumamosi.

Jeneza la Mandela hata hivyo lipatapelekwa kwa ndege nyumbani kwao katika kijiji cha Qunu mkoa wa Western Cape mnamo siku ya Jumapili kwa mazishi.

Mazishi ya Mandela yatakuwa kikomo cha maombolezi ambayo yamefanyika kwa siku kumi tangu aage dunia tarehe 5 Disemba.