Mazishi ya Mandela: Kauli yako

Image caption Mazishi ya Mandela yalipeperushwa moja kwa moja kwa televisheni Afrika Kusini

Maelfu walihudhuria mazishi ya Mandela wakatoa kauli zao na wewe pia tulikupa fursa kutoa ujumbe wako kupitia ukurasa wa facebook wa bbcswahili

13:42 Jeneza la Mandela hatimaye lateremshwa kaburini

13:25 Clement Ntukula kupitia Facebook ansema : Pumzika Kwa Amani Mzee Wetu Mandela Kazi Yako Itakumbukwa Daima

13:10 Hafla itakayofanyika kaburuni itahduhuriwa tu na jamaa na familia ya Mandela, viongozi wa ANC na maafisa wa AU, viongozi kumi na tano wa kitamaduni , viongozi wa kidini na maafisa wengine.

13:05 Askofu mkuu Desmond Tutu, ambaye alialikwa kwenye mazishi dakika za mwisho ni miongoni mwa wale wanaoelekea katika sehemu atakapozikwa Mandela kushiriki hafla itakayofanyika kaburini.

13:00 Wanajeshi wamebeba jeneza la Mandela kuondoka ukumbini kuelekea kwa maziko

Katambi James kutoka Dar es Salam kwenye ukurasa wa facebeook wa bbcswahili anawashukuru viongozi wote duniani kwa kujitokeza kuuaga mwili wa kiongozi mwenzao. Waendelee kuwa na moyo wa kujituma. Na kuacha majungu.

Ernest Mhando kupitia ukurasa wa facebook amesema kuwa Mungu ametowa na Mungu amemtwaa,ailaze mahali pema Roho ya shujaa wa Afrika Nelson Mandela mbinguni amen.

12:01 Kaunda ambaye anakaribia umri wa miaka 90 aliwashangaza wengi kwa kukimbia ukumbuni

12:00 Rais wa zamani wa Zambia Keneth Kaunda, ahutubia watu akitoa kumbukumbu zake kuhusu Mandela..alisema lazima wananchi wa Afrika Kusini wakumbuke kuwa ni muhimu kuendeleza sera za Mandela ikiwemo kuwapenda jirani zao kama wanavyojipenda wenyewe

11:50 Rais Jacob Zuma amemaliza kuwahutubia umati uliofika kwa mazishi ya Hayati Nelson Mandela kwa kauli kuwa Madiba atakumbukwa sana kwa sababu ya nafasi aliyokuwa nayo katika maisha yao. Pia amewataka wananchi kuendeleza urithi wa Mandela na sera zake

11:45 Ahmed Kathrada, aliyekuwa mfungwa wa kisiasa pamoja na Mandela, alitoa hotuba iliyovutia hisia. Alisema maisha yake sasa yamekuwa na pengo ambalo hajui nani anaweza kulijaza kufuatia kifo cha Mandela.

11:42 Mjukuu wa Mandela Nandi naye alisema babu yake aliwafunza kuwa wanaweza kuafikia chochote wanachokitaka maishani mwao

11:40 Naye Rais wa Malawi, Joyce Banda, alisema kuwa Mandela aliwafunza waafrika wote kuwa kwa ushujaa na imani mtu yeyote anaweza kuangamiza maasi katika jamii.

11:38 Naye waziri mkuu wa Ehiopia,Hailemariam Desalegn alisema kuwa wale wanaosherehekea maisha ya Mandela, lazima wafuate maadili aliyofunza na ambavyo alivyoishi maisha yake kwa kupigania uhuru na usawa.

11:36 am: Mlagwa Ngasala kupitia kwa ukurasa wa facebook anasema kuwa : Ki ukweli Mandela alikuwa mtu wa pekee mwenye maamuzi ya busara hakuwa na kinyongo mwepesi wa kusamehe yatupasa tuige mifano yake japo ni ngumu kuiga tabia ya mtu hasa ukarimu wengi tumekuwa tukishindwa, pumzika salama mzee Madiba.